Radio Uhai Description
Redio Uhai ni kituo cha Ukristo kinachotanganza kwa lugha ya Kiswahili kinachopatikana Tabora, Tanzania. Katika masafa ya 94.1 FM. Kituo hiki cha redio kina kusudi kuu la kuhubiri habari njema ya injili ya Yesu Kristo na kucheza nyimbo zenye heshima kwa Mungu. Hivi sasa, kuna vipindi zaidi ya thelathini zinazoelimisha nazo ni; Habari, kufundisha neno la Mungu, na vipindi vya familia, wanawake, na watoto. Tunatoa pia huduma kwa jamii katika masuala mbali mbali ya maendeleo. Vipindi hivi vimetengenezwa kusaidia watu katika maisha yao ya kila siku. Tunaamini redio ni zana nzuri ya kufikia maelfu ya watu katika mji wa Tabora na miji iliyo karibu na nje ya nchi kwa watu wanaozungumza kiswahili. Tangu Redio Uhai imeanza kutumika katika eneo la mji wa Tabora, maisha ya watu wengi yamebadilishwa na wengi wamempokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yao.
Open up
Comments about Radio Uhai Android Version